R ni nini?

R ni nini?

R ni lugha ya kikompyuta na mazingira yaliyo tengenezwa mahsusi kwa ajili ya kazi za kitakwimu (statistical computing) na picha maelezo (visualization). Mfumo huu ulihasisiwa na Ross Ihaka na Robert Gentleman  katika Chuo Kikuu cha Auckland, New Zealand na kwasasa hivi unaendelezwa na R Development Core Team. Mfumo wa R Ulitokana na lugha ya kikompyuta iliyoitwa S iliyovumbuliwa katika maabara za BELL miaka ya 80 washiriki wakiwa Rick Becker, John Chambers na Allan Wilks. Mfumo huu unafuata mfumo wa leseni ya “GNU General Public License” toleo la 2 na kuendelea kama zinavyochapishwa na Free Software Foundation hivyo basi kuufanya upatikane bure na hauna vikwazo vyovyote katika matumizi yake, yaani una uhuru wa kuutumia au kuusambaza kadri unavyotaka bila kukiuka kanuni zozote za leseni za matumizi.

Continue reading

Simika R na R Studio Kwenye Kompyuta Yako (R Installation)

Malekezo ya Video

Tafadhalia angalia video ifuatayo kabla ya kuanza zoezi hili, video hii inapatikana Youtube katika “Channel” ya EDx  Karolinska.

Kwa wenye uzoefu wa kusimika mifumo kwenye kompyuta

Kama una uzoefu wa kusimika mifumo kwenye kompyuta (software installation) unachotakiwa kufanya ili kuiwezesha kompyuta yako kuwa na mfumo wa R ni kushusha/kupakua na kusimika mifumo ifuatayo:

Zingatia:

  • Hifadhi mafaili ya mifumo uliyopakua sehemu ambayo utaikumbuka kuifikia
  • Kama una toleo la nyuma la mfumo wa R liondoe
  • Unashauriwa ufunge mifumo mingine uliyofungua kabla ya kuanza kusimika R
  • Simika R kwa kubofya mara mbili “double click” faili uliloshusha na kuchagua maelekezo yafuatayo:
    • Standard Windows installer
    • Put R in Your Start Menu
    • Place an R Icon on Desktop

Kwa wasio wazoefu

Tafadhali fuatilia maelekezo yafuatayo hatua kwa hatua.

Continue reading