Simika R na R Studio Kwenye Kompyuta Yako (R Installation)

Malekezo ya Video

Tafadhalia angalia video ifuatayo kabla ya kuanza zoezi hili, video hii inapatikana Youtube katika “Channel” ya EDx  Karolinska.

Kwa wenye uzoefu wa kusimika mifumo kwenye kompyuta

Kama una uzoefu wa kusimika mifumo kwenye kompyuta (software installation) unachotakiwa kufanya ili kuiwezesha kompyuta yako kuwa na mfumo wa R ni kushusha/kupakua na kusimika mifumo ifuatayo:

Zingatia:

 • Hifadhi mafaili ya mifumo uliyopakua sehemu ambayo utaikumbuka kuifikia
 • Kama una toleo la nyuma la mfumo wa R liondoe
 • Unashauriwa ufunge mifumo mingine uliyofungua kabla ya kuanza kusimika R
 • Simika R kwa kubofya mara mbili “double click” faili uliloshusha na kuchagua maelekezo yafuatayo:
  • Standard Windows installer
  • Put R in Your Start Menu
  • Place an R Icon on Desktop

Kwa wasio wazoefu

Tafadhali fuatilia maelekezo yafuatayo hatua kwa hatua.

Ili uweze kujifunza R vizuri nashauri usimike R kwenye kompyuta yako. Kitendo hiki kinafanana na namna unavyo fanya “installation” ya “apps” kwenye “smartphone” yako. Kitendo hiki kitakuwa na hatua nne:

 • Kushusha (download) mfumo mama wa R (base)
 • Kusimika (installation) mfumo mama wa R (base)
 • Kushusha mfumo mbele R Studio
 • Kusimika mfumo mbele R Studio

Shusha R

Kushusha R kuna hatua zifuatazo:

 • Tembelea wavuti ya R,
 • Chagua “server” yenye mfumo wa R iliyo karibu na eneo lako kijiografia kutoka katika mtandao wa “servers” zenye mfumo wa R duniani (CRAN).
 • Chagua “Operating System” ya kompyuta yako,
 • Chagua mfumo mama (base),
 • Shusha mfumo wa R

 

Utapata R kwa kutembelea tovuti ya mradi wa R – The R Project for Statistical Computing. Bofya picha ili kuikuza na ionekanae vizuri.

Capture2

CRAN ni mtandao wa “servers” zinazotunza mfumo wa R duniani, hivyo basi baada ya kubofya CRAN chagua sehemu yoyote iliyo karibu na Tanzania, nashauri ushushe kutoka Afrika ya Kusini (South Africa).

Katika ukurasa wa CRAN chagua mfumo wa R kutokana na aina ya “Operating System (OS)” iliyoko kwenye kompyuta yako, mfano kwa mimi natumia kompyuta yenye OS ya “Windows” hivyo basi nitachagua Download R for Windows, angalia mchoro hapo chini unavyoelekeza.

CRAN PAGE
CRAN PAGE

Katika ukurasa unaofuata chagua “base” huo ndio mfumo mama wa R unaotakiwa kutangulia kuwekwa, mfumo mama una vitu vya msingi vya kukuwezesha kufanya uchambuzi wa data, angalia kielelezo kichafuata.

RBaseSoftware

Hatua inayofuata ni kushusha mfumo wa R na kuifadhi kwenye kompyuta yako, angalia kielelezo kinachofuata.

R4Windows

Hifadhi mfumo wa R kwenye kompyuta yako, hakikisha unafahamu mfumo wa R unahifadhiwa sehemy gani ya kompyuta yako(mfano, “Desktop”, “Documents” au “Folder ” lililo sehemu nyingine yoyote ya kompyuta yako). Fuatilia kielelezo kifuatacho.

SaveR

 

Subiri kompyuta yako imalize kushusha mfumo wa R, muda wa kusubiri utategemea spidi ya muungo wa kompyuta yako kwenye mtandao wa kimataifa wa mawasiliano ya kikompyuta (Internet connection speed).

——> ITAENDELEA

 Marejeo

 1. Installing R and RStudio – John Fox
 2. Introduction to the R Statistical Computing Environment – John Fox
 3. R Manuals – R Installation and Administration
 4. Youtube

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s